Announcement

KILIMANJARO CHRISTIAN MEDICAL UNIVERSITY COLLEGE

A constituent College of Tumaini University Makumira

Tangazo la mahafali ya mwaka 2019

Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba cha Kikristo Kilimanjaro (KCMUCo),

 anayo furaha kuwaalika wahitimu wa mwaka 2019, familia zao na marafiki, kuhudhuria sherehe za mahafali ya 20 yatakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 16, Novemba 2019. Mahafali hayo yataanza saa 3 asubuhi chuoni hapo kwa maandamano ya kitaaluma.

Mahafali yatatanguliwa na Kongamano (Convocation) litakalofanyika siku ya Ijumaa tarehe 15 Novemba 2019 kuanzia saa 8 mchana katika ukumbi wa MD 1 ulioko Chuoni hapo.

Aidha, mazoezi ya mahafali yatafanyika siku hiyo ya Ijumaa tarehe 15 Novemba 2019, baada ya kongamano.

Wahitimu watakaoshiondwa kushiriki mazoezi  haya hawataruhusiwa kushiriki mahafali.

Wahitimu wawasiliane na ofisi ya mkuu wa chuo kuthibitisha ushiriki wako mapema kwa; simu na. 0754831901, 0714532705 au kwa Barua Pepe ya: info@kcmuco.ac.tz

Wale ambao hawatathibitisha, hawataruhusiwa kushiriki mahafali haya.

Majoho ya mahafali yataanza kutolewa wiki moja kabla ya mahafali.

NYOTE MNAKARIBISHWA.

imetolewa na

Ofisi ya Mkuu wa Chuo KCMU College.